Baba Levo awachana Diamond na Alikiba “Kama hawataki kuelewana waendelee kugombana sisi tule hela zao”

Msanii na diwani wa kata ya MWANGA Ujiji Kigoma mjini Baba Levo ameongea akijivua kuwa mkoa wa Kigoma kuwa na vijana wenye vipaji lakini akiwashauri Ali Kiba na Diamond kuwa “waachane na tofauti zao waijenge Kigoma ila kama hawataki basi wavurugane sisi tupige pesa kwenye mashow yao “

Mbali na hilo amemtaka Peter Msechu kumlipa hela zake lakini amezungumzia kuhusu ugomvi uliodaiwa kuwepo kati ya Shilole na mume wake Uchebe

Mwanamuziki Drake Aanika Chanzo bifu na Chris Brown

RAPA Aubrey Graham maarufu kwa jina la Drake, amefunguka kwa mara ya kwanza chanzo cha mgogoro wake dhidi ya mkali wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown.
Drake amesema wawili hao waliingia kwenye mgogoro kwasababu ya Rihanna, lakini anashukuru kila kitu kwa sasa kipo sawa na wamefanikiwa kufanya muziki wa pamoja.
“Chris alikuwa kwenye uhusiano na Rihanna kwa kipindi kirefu hadi wanakuja kuachana mwaka 2009, baada ya kuachana nikawa rafiki wa karibu na Rihanna jambo ambalo halikuwa sawa kwa Chris, lakini hakukuwa na kitu chochote kibaya na ndio maana kwa sasa sina tofauti na Chris.
“Ukweli ni kwamba wanawake wamekuwa sababu kubwa ya migogoro, nadhani kwa sasa Rihanna atakuwa anaumia akiwa anaona au kusikia kuwa nipo karibu na Chris,” alisema msanii huyo.

Mahakama ya Angola imeagiza mali za mtoto wa rais zikamatwe

MAHAKAMA ya Angola imeagiza kukamatwa kwa mali na akaunti za benki za bilionea ambaye ni binti wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo Dos Santos, Bi Isabel Dos Santos.
Kukamatwa kwa mali hizo kunatokana na mipango ya serikali iliyopo kukabiliana na ufisadi katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.
Utawala wa Rais Joao Lourenco unataka kuchukua takriban dola bilioni moja ambazo umekuwa ukimdai Bi Isabel Dos Santos na washirika wake.
Amepinga madai hayo na kusema kwamba hajafanya makosa yoyote wakati babake alipokuwa mamlakani.
Akidaiwa kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika, Bi Dos Santos anakadiriwa na jarida la Forbes kuwa na mali yenye thamani ya dola bilioni 2.2.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 anaishi ughaibuni, akisema kwamba aliondoka Angola kwa kuwa maisha yake yalitishiwa.
Anaendesha biashara kubwa akiwa na kampuni nchini Angola na Portugal ambapo anamiliki hisa katika kampuni ya Nos SGPS.
Mahakama iliagiza mali ya Bi Santos kupigwa kuchukuliwa ikiwemo akaunti zake za benki mbali na hisa zake katika kampuni nchini Angola, ikiwemo ile ya Unitel na Benki ya Fomento de Angola (BFA) kilisema chombo kimoja cha habari cha serikali ambapo naye alisema anashutumu kile alichokitaja kuwa shambulio linaloshinikizwa kisiasa.

Kuhusu BENDERA iliyokuwa Ikipepea Wakati wa Mapokezi ya Msanii Diamond Platnumz Kigoma Ilimaanisha Nini

Kuna tuhuma tatu kuhusiana na muonekano wa bendera hiyo, tutawaorodhesha hapa tuhuma hizo na kuzichambua.
Tuhuma ya kwanza inasema:

-Watu wa Kigoma ni washamba na hawajasoma, Bendera inayo onekana hapo ni bendera ya nchini Uingereza (United Kingdom) iweje ipeperushwe na ilihali wana Kigoma sio waingereza?

#JAWABU
Bendera hiyo siyo ya nchini uingereza na wala haina unasaba na uingereza, kumbuka bendera ya uingereza imeundwa kwa mfumo wa (Union Jack) yaani mistari yote imekutana kwenye msaraba mwekundu, lakini hii iliyoonekana imeundwa kwa mfumo wa (Union face) kwa maana katikati ya bendera kuna picha ya mlengwa ambae ni Diamond ikimaanisha watu wameungana na kukusanyika kwa ajili yake, na wala hakuna msaraba mwekundu kama bendera ya UK.
Tuhuma ya pili inasema
-Bendera inayoonekana ni bendera ya kishetani inayomilikiwa na Freemason huko Kigoma na ndio imekusanya nguvu ya watu hao.

#JAWABU.
Si kweli, kwasababu bendera ya freemason haiko union, yenyewe ina rangi ya Blue na Njano au Blue na Gold Compass Masonic Flag. Nasio hii iliyoonekana hapa Kigoma. Ni kweli mnamo sep 5, 2017 kijana Emmanuel Songoye aliuwawa kwa kuchomwa moto na wananchi huko Kabanga, kasulu akihofiwa kuwa ni Freemason kutokana na mali zake, lakini haina uhusiano wowote na bendera hii hata kidogo.
Tuhuma ya tatu inasema
-Bendera inayoonekana ni bendera ya kichawi iliyokuwa ikiwaongoza watu bila kujijua kwa maana watu wote walionyoosha mikono juu pia walifungua viganja vyao vya miko (yaani vidole vyote vya mikono vilikunjuka kwa watu wote),
#JAWABU
Si kweli, hii bendera haijatumika kama ushirikina au uchawi kuongoza watu, mkumbuke wakati watu wananyoosha mikono juu walikuwa wakiimba kwa kuwapungia mikono wasanii waliokuwa upande wa jengo la station ghorofani, sasa kikawaida huwezi kumpungia mtu mkono ilihali umekunja ngumi, ni maswala ambayo hayaingii akilini.

UHALISIA WA BENDERA
Bendera hii imechorwa kama bendera ya ulaya ‘United Kingdom’ kwa maana ya muonekano wa rangi zake, kwakuwa Kigoma iliungana kumpokea Diamond basi hakuna budi kuitwa ”Kigoma United for Diamond Platinum” au unaweza kuita ”United Kigoma” badala ya ”United Kingdom”. Mchoraji ameondoa Kingdom na kuweka Kigoma kwasababu katikati ya bendera ameweka picha halisia ya msanii Diamond Platinumz.

Uwanja wa Simba Bunju kuanza Kutumika Mechi za Ligi

Simba imethibitisha kuwa uwanja wao wa Mo Simba Arena, uliopo Bunju utaanza kutumika kwenye michuano ya ligi kuu ya soka ya wanawake Tanzania Bara.

Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa mchezo wa leo kati ya timu ya Simba Queens dhidi ya Kigoma Sisters utapigwa Mo Simba Arena.

‘Timu ya Simba Queens leo inacheza mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi ya Kigoma Sisters. Mchezo huo unapigwa kwenye uwanja wa Mo Simba Arena kuanzia saa 10:00 jioni’, imeeleza taarifa hiyo.

Ikumbukwe Uwanja wa Mo Simba Arena wenye viwanja viwili ambavyo pia vinatumika na timu ya wanaume ya Simba kufanyia mazoezi, ulipokelewa na klabu pamoja na mashabiki kutoka kwa mkandarasi Desemba 7, 2019.

India: Chuo Kikuu kufundisha madaktari masuala ya uchawi na mizimu

Chuo maarufu nchini India kimeanza kutoa kozi ya ngazi ya cheti kwa madaktari jinsi ya kutibu wagonjwa wanaopatwa mapepo au huyaona.

kozi hiyo ya miezi sita katika chuo kikuu cha Banaras Hindu (BHU) kwa mji wa kaskazini wa Varasanasi, kozi hiyo itaanza mwezi Januari.

Na pia kozi hiyo itakua inatolewa na kitengo cha afya ya akili na magonjwa yasiyo ya kawaida.

Msemaji wa chuo aliambia shirika la habari la India kuwa kitengo cha masomo ya uchawi kimeanzishwa.

”Kitengo hicho kinaitwa Bhoot Vidya na kunajihusisha na magonjwa yasiyo ya kawaida ama matatizo ya akili” anasema Yamini Bhushan Tripathi mkuu wa kitengo hicho.

Aliongeza pia Chuo hiki ndo chuo cha kwanza kuanzisha kozi ya namna hiyo ambayo itafundisha masomo ya utabibu wa majini, mapepo na mizimu.

Matibabu yatatolewa kwa njia ya dawa za asili, miti shamba na masaji.

Kwa mujibu wa utafiti wa 2016 wa kitengo cha magonjwa ya akili (Nimhans) karibu asilimia 14 ya watu nchini India ni wagonjwa wa akili na mwaka 2017 shirika la afya duniani WHO inakadiria asilimia 20 ya Wahindi wanaweza kupatwa na msongo wa mawazo katika kipindi fulani katika maisha yao.

Lakini kuna chini ya wagonjwa 4,000 wa akili huwa wanaenda hospitali kupatiwa matibabu rasmi, kuna uelewa mdogo sana juu ya afya ya akili.

Lakini pia kutokana na unyanyapaa kusambaa sana , wagonjwa wachache ndio wanaenda hospitali wengi huenda kwa waganga wa kienyeji na kudhani kuwa watatibiwa matatizo yao ya akili.

Wengi wameonesha kulidhihaki tangazo hilo katika mitandao ya kijami, baadhi wameuliza serikali ya India je vipaumbele vyake vikwapi?

Taarifa ya kuwa chuo hiko cha serikali kitaanza kutoa kozi hiyo imepokelewa kwa maoni mbalimbali katika mitandao ya kijamii, wengi wakiuliza ni namna gani kozi hiyo itatolewa?

Baadhi ya watu wanasema kozi hiyo ingepewa jina kabisa.

Faru Vicky atangazwa mrithi wa kiti cha Faru Fausta ‘Bibi wa kreta’

Kufuatia kifo cha aliyekuwa faru mwenye umri mkubwa zaidi duniani, Fausta, Mamlaka ya eneo la Ngorongoro (NCAA), imemtangaza faru Vicky kuwa faru mwenye umri mkubwa zaidi nchini.

Faru Vicky anakadiriwa kuwa na miaka 49 kwa sasa na hivyo kuwa faru pekee anayeweza kukalia kiti cha Fausta ambaye alikufa akiwa chini ya uangalizi maalumu ndani ya bonde la Ngorongoro akiwa na miaka zaidi ya 57, na kuacha rekodi ya kuwa faru mweusi mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani.

Mwili wa Faru Fausta kuhifadhiwa kama kivutio cha utalii
Kamishna wa uhifadhi katika mamlaka ya Ngorongoro, Dkt. Freddy Manongi amesema kwakuwa faru Fausta alikuwa akiishi ndani ya jengo maalumu, mamlaka ya Ngorongoro inafikiria pia kumhamishia faru Vicky ndani ya nymba ya marehemu Fausta ili kumsaidia na yeye katika kipindi cha uzee.

Ikumbukwe kuwa faru wnakadiriwa kufikisha umri wa miaka 35 hadi 40 wakiwa porini na huishi zaidi ya hapo wakiwa chini ya uangalizi maalumu.

Mtoto Mdogo Afariki Kwa Kula Kitimoto

Watu wawili wa Familia moja (Baba na Mtoto) wanashikiliwa na Polisi Mkoani Rukwa kufuatia kuwauzia Wanakijiji nyama ya nguruwe ambae alikuwa mzoga na kusababisha Mtoto wa miaka miwili Mariam Peter kufariki Dunia huku Watu wengine 16 wakikimbizwa Zahanati katika Kijiji cha Utengule Wilayani Kalambo, Rukwa .

Familia ya Osward Simpungwe ilichinja nguruwe ambae alikufa mwenyewe bila kujua kilichomua na kuuza nyama ambayo iliwaletea madhara walaji.

Mtoto Mariam aliumwa tumbo baada ya kula nyama hiyo iliyonunuliwa na Baba yake na akafariki wakati akikimbizwa Zahanati.

“Matukio ya kulishwa mizoga yanajirudia mara kwa mara hapa, Serikali ituletee Wataalam wa kukagua nyama kabla ya kuliwa”– Mwanakijiji

Diamond Ajenga Msikiti Nyumbani Kwao KIGOMA Auzindua Kwa Kupanda Mti

Diamondplatnumz Akipanda Mti Nje ya Msikiti Alioujenga Mwenyewe, Uliopo Ujiji Unaoitwa MASJID AL-AZIZ na Utatumiwa na waislam Wote Katika Ibada, Hii Ikiwa Sehemu yake ya Kurudisha Kwenye Jamii Kidogo Alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu Katika Kipindi Chote Alichofanya Sanaa

Na Hapa ni kwao kwa Msanii Diamondplatnumz na Huu ndio msikiti ambao msanii Diamond Ameujenga kwaajiri ya Wanakijiji wenzake katika mtaa wa Eneo lao… Mwenye Mungu Ambariki Diamond Katika Hili… Wote katika Imani Tuseme **AMIIN